“Everyone wants to live at the top of the mountain, but all the happiness and growth occurs while you’re climbing it.” – Andy Rooney
Wale waliofanikiwa sana wanatufundisha somo kubwa kuhusu mafanikio kupitia maisha yao.
Wengi huanzia chini kabisa na hapo kujisukuma kufanya kazi usiku na mchana ili kufika kwenye kilele cha mafanikio.
Lengo likiwa ni wakishafika kileleni, yaani kufikia uhuru wa kifedha, basi waweze kustaafu na ‘kula bata’ kwa kipindi cha maisha yao kilichosalia.
Watu hao huanzisha biashara na kupambana kuzikuza na hatimaye kufanikiwa kuziuza.
Katika kuuza biashara zao hizo wanapata fedha nyingi ambazo zinawawezesha kustaafu ns kuendesha maisha yao kwa kipindi chote kilichobaki hata kama hawatafanya kazi tena.
Wanafurahia hilo, wanachukua likizo yao ya kwanza na kwenda matembezini kula maisha.
Lakini kabla hata mwezi haujaisha, wanagundua furaha haipo kwenye kula maisha.
Japo wakati wanapambana kukuza biashara zao waliona ni kitu kigumu, lakini ndiyo wakati walikuwa na furaha kuliko hata wakati wa mapumziko.
Hivyo wengi humaliza likizo na badala ya kustaafu wanaenda kuanzisha biashara mpya.
Kupitia maisha ya hawa waliofanikiwa sana, tunajifunza kwamba furaha haipo kwenye kilele cha mafanikio, bali ipo kwenye hatua unazopiga kufika kwenye kilele hicho.
Hivyo kama unataka kupata furaha ya kudumu kwenye maisha yako, jiandae kwa haya mawili;
Kwanza fanya kile unachopenda kufanya, kile kinachotoka ndani yako kweli, kile ambacho uko tayari kukifanya hata kama hulipwi.
Pili usikimbilie kustaafu na kutaka mapumziko ya milele baada ya kufika kwenye kilele cha mafanikio. Endelea kuweka juhudi kila siku, maana furaha ni matokeo ya juhudi unazoweka.
Kama kile unachofanya sasa siyo unachopenda, basi jitume zaidi usiku na mchana, upate uhuru wa kifedha na ukishastaafu kwenye hicho, uende kufanya kile unachopenda.
Mchango wetu binadamu ni kupitia kile tunachofanya, hivyo kama hakuna tunachofanya, tunaona maisha yetu hayajakamilika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kutumia fursa kama kisingizio cha kutoroka, fungua hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/17/2025
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
Asante Sana kocha kwa somo zuri kupitia tafakari ya leo,nimekuwa naona watu wa jamii tofauti tofauti na mitindo yao ya maisha,wazungu wengi wao wao wanafanya kazi kwa maisha yao yote, kazi zingine kama sehemu ya furaha yao.ila hapa kwetu nadhani ni ukosefu wa Maarifa watu wanapenda sana starehe,kupumzika hata kama hawana chochote walichonacho.napenda sana kujifunza na kuongeza maarifa mapya kila inapobidi.
LikeLike
Vizuri Beatus.
LikeLike