Watu wengi hawajafanikiwa na wengi zaidi hawatafanikiwa kwa sababu wanakosa viungo viwili muhimu sana kwenye mafanikio ya aina yoyote ile.

Kiungo cha kwanza ni msimamo, kufanya jambo kwa kurudia rudia bila ya kuacha. Hili linaonekana wazi, ukiangalia waliofanikiwa, huwa wamefanya kitu hicho kwa muda mrefu. Lakini waangalie walioshindwa, katika kipindi hicho hicho wamejaribu vitu vingi na kuacha. Wanaanza kitu kipya, baada ya muda wanakiacha na kuanza kingine. Bila ya msimamo, bila ya kuchagua kitu kimoja au vichache na kujiambia unakwenda kuweka kila kitu kwenye vitu hivyo, mafanikio yatakuwa magumu kwako.

Kiungo cha pili ni uvumilivu. Kinachopelekea wengi kukosa msimamo ni kuchelewa kwa matokeo. Umesikia watu wanasema kitu fulani kinalipa, unajaribu mara ya kwanza hakikulipi, unaacha na kwenda kufanya kingine. Kila kitu huwa kinalipa, lakini siyo kila kitu kinalipa mara ya kwanza kukifanya. Kuna vitu vinakuja kulipa baada ya kuvifanya kwa muda mrefu. Hivyo uvumilivu ni muhimu sana, lazima uwe tayari kusubiri, lazima uvumilie matokeo usiyoyataka, huku ukikazana kuwa bora zaidi.

Hakuna kitakachokushinda unapokuwa na msimamo na uvumilivu, unapofanya bila ya kuruhusu sababu yoyote ikuzuie na unapokuwa na subira hata kama matokeo unayopata siyo uliyotegemea. Fanya maamuzi na jipe muda, weka juhudi na kazana kuwa bora kila wakati na mwisho wa siku, utapata matokeo mazuri.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha  

Normal
0

21

false
false
false

SW
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,sans-serif;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-language:EN-US;}