“No person hands out their money to passersby, but to how many do each of us hand out our lives! We’re tightfisted with property and money, yet think too little of wasting time, the one thing about which we should all be the toughest misers.” – Seneca.
Ukikutana na mtu njiani akakuambia umpe shilingi laki moja, au hata elfu 10 tu, hutakimbilia kumpa.
Lazima uhoji kwa nini unapaswa kumpa fedha hiyo.
Kwa maneno mengine huwa tuna ubahili mkubwa kwenye fedha na mali zetu,
Huwa tunazichunga zisipotee kwa namna yoyote ile.
Sasa njoo kwenye muda, ni mara ngapi umewaruhusu watu wachezee na kupoteza muda wako?
Unafanya kazi na mtu anakupigia simu kwa jambo lisilo muhimu, unaacha kazi na kujibu simu yake.
Unatembelea mitandao ya kijamii na kuzurura huko kwa muda mrefu, hakuna unachopata na unapoteza muda wako.
Kwa kifupi, unatapanya na kuchezea muda wako.
Ukilinganisha fedha na muda, kipi muhimu?
Ukipoteza fedha, unaweza kupata nyingine.
Lakini ukipoteza muda ndiyo imetoka, huwezi kuupata tena.
Hivyo muda ni muhimu na adimu kuliko fedha.
Kama tunataka kuwa na ubahili, basi ubahili wa muda ni muhimu kuliko wa fedha.
Anza sasa kulinda muda wako,
Kwanza kabisa anza kwa kuupa thamani ya fedha.
Kila dakika yako moja, ipe thamani ya fedha.
Kisha kabla hujafanya kitu, jiulize kama kweli kina thamani sawa na muda wako.
Mfano kama umeipa dakika yako moja thamani ya shilingi elfu moja, unapaswa kuitumia kila dakika yako kwa vitu vinavyokuingizia au kuokoa kiasi hicho cha fedha.
Hivyo unapotaka kutembelea mitandao ya kijamii au kufuatilia habari, utajiuliza kwanza kama kufanya hivyo kunakuingizia fedha.
Kama siyo, usifanye.
Kuwa bahili na muda wako, hayo ndiyo maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu yale tunayojisumbua nayo sasa ambayo baadaye watu wakiyaangalia watacheka, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/15/2054
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante Sana kocha kwa,ni kweli muda ukipotea umepotea,tunatakiwa muda wetu kuupa thamani kubwa sana.
LikeLike