“Anyone who is engaged in really important things is very simple because he does not have time to create unneces sary things.” – Leo Tolstoy
Kama huna muda, kama kila wakati uko bize na hupati nafasi ya kufanya yale muhimu kwako,
Basi jua kuna mahali unakosea,
Kuna mambo yasiyo muhimu unahangaika nayo,
Kuna maisha yasiyo yako unayoyaiga.
Kila anayefanya yaliyo muhimu kwake na kupuuza yasiyo muhimu, huwa ana muda wa kutosha na maisha yake huwa ni rahisi.
Hiyo ni kwa sababu anakuwa hana muda wa kufanya vitu visivyo na umuhimu kwake.
Unapoanza kuhangaika na vitu visivyo muhimu, unatengeneza matatizo mapya kwenye maisha yako na hayo yanakuweka bize kweli kweli.
Unakuja kustuka uko bize wakati hakuna muhimu unachozalisha au kukamilisha.
Ni wakati sasa wa kufanya palizi kwenye maisha yetu,
Wakati wa kuondoa magugu ambayo yanatuweka bize huku tukiwa hatupigi hatua kubwa.
Tafakari maisha yako, kule ulikotoka mpaka ulipo sasa, angalia pia kule unakotaka kufika.
Tafakari kila unalofanya kwenye siku yako, kila unalohangaika nalo.
Kisha jiulize kama yale umekuwa unasumbuka nayo huko nyuma yamekufikisha wapi?
Pia jiulize hayo unayosumbuka nayo sasa kama yatakufikisha kule unakotaka kufika.
Bila kufanya palizi kwenye shamba, magugu yanazidi mimea nguvu na inashindwa kuzalisha vizuri.
Bila kufanya palizi kwenye maisha yako, yasiyo muhimu yanakuzidi nguvu na unashindwa kupiga hatua
Ondoa kila gugu la yasiyo muhimu kwenye maisha yako, utabaki na machache ya kufanya na hivyo kuwa na muda wa kutosha.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu ndoano ya kunasa umakini wako, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/20/2059
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante Sana kocha kwa tafakari hii, ukweli kila Mara kuna umuhimu wa kujifanyia tathimini,hata hatua tunazopiga wakati mwingine zinaweza kukudanganya ukadhani uko sahihi.
LikeLike
Karibu Beatus.
LikeLike