“One hour of honest, serious thinking is more precious than weeks spent in empty talks.” – Leo Tolstoy

Watu wengi wanapenda kutumia muda wao mwingi kuongea kuliko kufikiri.
Wengi hawapendi kabisa kufikiri,
Hivyo mtu anapohitajika kufikiri, atatafuta kila namna ya kukimbia jukumu hilo.

Saa moja ya kufikiri kwa kina ni bora kuliko wiki nzima ya kuongea maneno yasiyo na maana.
Saa moja ya kifikiri kwa kina ina manufaa kwako kuliko wiki nzima ya kuzurura mitandaoni.

Kinachopelekea wengi kujikuta kwenye changamoto na kukwama, ni kutokufikiri.
Kila mtu anakazana kuongea na kutoa maoni yake, kwa mazungumzo ya kawaida na mabishano ya mitandaoni.
Mtu anajikuta amechoka na hakuna hatua anayopiga.

Huwezi kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako kama hupati muda wa kufikiri kwa kina,
Muda wa kuwa peke yako kwenye utulivu wa hali ya juu na kisha kufikiri kwa kina na kuangalia pande zote za hali husika.

Ndani yako kuna vitu vingi,
Majibu mengi unayotafuta sasa tayari yako ndani yako.
Lakini huyafikii kwa sababu hupati muda wa kufikiri kwa kina.
Ipe kufikiri kipaumbele kikubwa kwenye maisha yako na utaona wazi fursa za wewe kupiga hatua zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu jinsi mipango ilivyo kama ramani, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/21/2060

Pia kama hujashiriki kwenye mjadala kuhusu maamuzi, fungua hapa ushiriki; http://www.mafanikio.substack.com/p/fanya-maamuzi-mara-moja-kisha-sahau

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.