“The truth is harmful only to evildoers. Those who do good love the truth.” – Leo Tolstoy

Ukweli huwa haubembelezi,
Huwa unabaki kuwa ukweli mara zote, bila ya kujali wengine wanaupokeaji.
Tabia hii ya ukweli imekuwa ni sumu kubwa kwa wale wanaotenda maovu.
Kwa sababu hata wajaribu kuuficha ukweli kwa gharama gani, siku moja ukweli unajiweka wazi.

Kwa wanaotenda wema, huwa wanaupenda ukweli, kwa sababu hakuna wanachoficha.
Kila wakati wako huru na ukweli unapojulikana ndiyo wanakuwa salama zaidi.
Wale wanaotenda wema wanaweza kusingiziwa na kutuhumiwa kwa mambo yasiyo kweli,
Lakini huwa wanajua ukweli haupotei, ipo siku utawaweka huru.

Kuwa upande wa ukweli, tenda wema mara zote na hutakuwa na cha kuhofia kwenye ukweli.
Utaupenda na kuukubali ukweli na hilo litakufanya uwe huru zaidi.
Usidanganyike na wale unaoona wanafanya maovu na ukweli haujulikani,
Ni swala la muda tu, ukweli huwa haufi na hata ukifichwa unafika wakati ambapo unakuwa haufichiki tena.

Ukitaka maisha yako yawe rahisi na huru, usiwe na chochote kiovu unachoficha.
Hata unapokosea, kueleza ukweli na kuomba samahani inakuweka huru.
Lakini kuficha kunapelekea kosa dogo kujengeka na kuwa kubwa, huku wewe ukikosa amani na uhuru.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu misingi midogo midogo 10 ya kuiishi kila siku ili kuwa na mafanikio makubwa, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/23/2062

Tafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.