Habari rafiki yangu mpendwa,

Napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha kwenye SOMA VITABU APP, ambayo ni njia bora ya kusoma vitabu mbalimbali kwa nakala tete.

SOMA VITABU APP inakupa nafasi ya kununua na kusoma vitabu kwenye simu au tablet yako, bila ya kuwa kwenye hatari ya kupoteza vitabu vyako.

Kwa sasa SOMA VITABU APP itakuwa na vitabu vilivyoandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.

App ni rahisi kutumia, rahisi kuchagua na kulipia kitabu na rahisi kusoma vitabu baada ya kuwa umevilipia.

MAELEZO YA KUTUMIA SOMA VITABU APP.

Hapa ni maelekezo ya jinsi ya kuweka na kutumia SOMA VITABU APP.

Jinsi ya kuinstall app ya SOMA VITABU.

 1. Ingia GOOGLE PLAY
 2. Sehemu ya search andika Soma Vitabu au bonyeza hapa kwenda moja kwa moja.
 3. Install app.
 4. Open baada ya kuinstall.
 5. Nenda kwenye app na bonyeza sehemu ya PROFILE kisha bonyeza REGISTER.
 6. Andikisha namba yako (uwe na line ya namba hiyo maana kuna code itatumwa)
 7. Ingiza code (Kama line ipo kwenye simu unayotumia itaingia yenyewe).
 8. Kamilisha usajili kwa kuandikisha majina na unapokaa.
 9. Rudi kwenye app na utaona vitabu mbalimbali.

Kwa maelekezo zaidi angalia video kwa kubonyeza maandishi haya.

Jinsi ya kununua na kusoma vitabu.

 1. Ingia kwenye app,
 2. Chagua kitabu unachotaka kununua.
 3. Bonyeza kitabu na nenda kwenye READ PREVIEW kuona kitabu kwa ufupi.
 4. Kununua kitabu bonyeza BUY NOW
 5. Itakupeleka kwenye MY BOOKS, bonyeza tena kitabu, itafunguka kisha bonyeza LIPIA KITABU.
 6. Chagua mtandao kati ya TIGO PESA, MPESA, AIRTEL MONEY au HALOPESA, Mtandao unaochagua uwe kwenye simu unayotumia app.
 7. Ruhusu App iweze kufanya malipo kwenye simu yako.
 8. Weka namba ya siri na itakamilisha muamala.
 9. Rudi kwenye MY BOOKS, utaona kitabu ulicholipia kimeandikwa NOT PAID.
 10. Kibonyeze na ingiza namba uliyotumia kulipia, ukishaingiza namba bonyeza THIBITISHA MALIPO.
 11. Baada ya muda kitabu kitakuwa kimethibitishwa na kitaandika PAID, hapo unaweza kukifungua na kukisoma.

Kwa maelekezo zaidi angalia video kwa kubonyeza maandishi haya.

Jinsi ya kuendelea kutumia app.

 1. Fungua app kwenye simu,
 2. Nenda kwenye MY BOOKS kusoma vitabu ulivyolipia.
 3. Kununua vitabu vingine bonyeza HOME.

Kwa maelekezo zaidi angalia video kwa kubonyeza maandishi haya. Au angalia video hapo chini.

Angalia maelekezo yote hapa ya jinsi ya kuweka na kutumia SOMA VITABU APP.

Kama unakwama popote kwenye kutumia app, wasiliana na 0678 977 007 kupata maelekezo zaidi.

Karibu kwenye SOMA VITABU APP, upate njia bora ya kusoma vitabu pamoja na usomaji rahisi wa vitabu vizuri vya mafanikio.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.