“Bad things are easy to do, good things are done only with work and effort.” — Dhammapada

Matapeli wana siri moja ya kuwanasa watu wanaotaka kuwatapeli.
Huwa wanafanya kitu kionekane kuwa rahisi kabisa kufanya.
Na kwa kuwa watu wanapenda urahisi, basi hunasa kwenye mitego hiyo na kutapeliwa.

Vitu vibaya na visivyo sahihi ni rahisi kufanya,
Vitu vizuri na vilivyo sahihi vinahitaji juhudi na kazi kuvifanya.
Hivyo pima usahihi wa chochote unachofanya kwa kuangalia ugumu wake.

Vitu rahisi kufanya pia haviwezi kukupa mafanikio makubwa, hata kama ni sahihi.
Hiyo ni kwa sababu kila mtu anavifanya.

Kuiga kile wengine wanafanya ni rahisi,
Lakini hilo halitakufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Kuwa wewe ni kugumu, lakini kutakupa mafanikio makubwa.

Usiwe mtu wa kukimbilia vitu rahisi, utatapeliwa na hata kupotea.
Kimbilia vile vilivyo sahihi, ambavyo mara zote huwa siyo rahisi kufanya.

Kuna vitu vingine ukiwa nje unaviona ni rahisi kufanya,
Ni mpaka uingie ndani ndiyo utaona ugumu wake,
Hivyo unapokutana na ugumu kwenye lolote unalofanya usikimbie, jua uko kwenye njia sahihi.
Na unapokutana na urahisi ambao haukusumbui usifurahie, jua uko kwenye njia isiyo sahihi.

Wanaofanikiwa sana ni wachache kwa sababu hao wako tayari kufanya yaliyo magumu.
Wanaoshindwa ni wengi kwa sababu wanakimbilia yale rahisi.
Chagua mwenyewe unataka ninim urahisi unaokupoteza au ugumu unaokupeleka kwenye mafanikio.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu aina ya watu unaowasikiliza, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/19/2089

Kwenye Mwongozo wa mafanikio kuna makala mbili fupi na nzuri,
Moja kuhusu masomo 25 ya maisha; https://mafanikio.substack.com/p/kutoka-kwa-robin-sharma-masomo-25
Nyingine kuhusu maswali ya kujiuliza unapopata wazo la biashara; https://mafanikio.substack.com/p/kutoka-kwa-seth-godin-maswali-kwa

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.