“Blaming others is an entertainment which some people like and cannot restrain themselves from. When you see all the harm this blaming causes, you see that it is a sin not to stop people from practicing this entertainment.” – Leo Tolstoy

Kuwalaumu wengine ni moja ya burudani ambayo wengi wanaipenda.
Unapomlaumu mtu mwingine, wajibu na makosa yanaenda kwake,
Wewe unabaki kuwa muathirika, ambaye maamuzi na hatua za wengine vimekuumiza.

Hii ni burudani kwa sababu inaficha ukweli, ukweli kwamba chochote unachowalaumu nacho wengine, wewe ndiye tatizo kuu.
Hivyo kama kuna mtu wa kwanza kumlaumu, ni wewe mwenyewe.

Burudani hii ya kurusha lawama kwa wengine huwa ina madhara makubwa.
Kwanza mtu anayelaumu anajivua uwajibikaji na kuwapa wale anaowalaumu.
Pia anayelaumu anajiona hana makosa, ni wengine ndiyo wamemfikisha pale alipo.

Ukweli wa maisha ni huu; popote ulipo na chochote kinachoendelea kwenye maisha yako, wewe ndiye unayewajibika
Kama kuna makosa yametokea, wewe ndiyo chanzo.
Hata kama watu wamekuonea na kukuibia, ni wewe mwenyewe umewapa nafasi hiyo.

Hivyo acha kulalamika au kulaumu wengine.
Beba jukumu la maisha yako,
Angalia ni wapi unakosea ili usirudie tena.
Maisha yako ni jukumu lako, usilikimbie kwa kutupa lawama kwa wengine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/26/2096

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.