“Temporary solitude from all things in this life, the medita tion within yourself about the divine, is food as necessary for your soul as material food is for your body.” – Leo Tolstoy

Huwa unaulisha mwili wako kila siku, lakini je unahangaika kuilisha rohk yako.
Kwa wengi, roho ni eneo lenye utapiamlo kwa sababu halilishwi kabisa au hata likilishwa basi ni vitu visivyo sahihi.

Na hata uchovu mkubwa ambao watu wanaupata (burnout) unachangiwa kwa kiasi kikubwa na roho kuwa na utapiamlo, kukosa chakula sahihi cha kiroho.

Kuilisha roho yako ni jukumu unalopaswa kufanyia kazi kila siku, kama unavyohangaika kulisha mwili wako.

Swali ni je unajua nini chakula cha roho yako?

Vyakula vya msingi kabisa vya roho yako na ambavyo ni vya afya ni hivi;
👉🏽Tahajudi, kuyatuliza na kuyadhibiti mawazo yako ni hitaji muhimu la kiroho.
👉🏽Kusali, kujinyenyekeza kwa nguvu iliyo kubwa kuliko wewe ni kitu kinachoipa roho yako nafasi ya kuungana na nguvu hiyo.
👉🏽Shukrani, kushukuru kwa kila ulichonacho na kinachoendelea kwenye maisha yako ni kuifanya roho yako ione utele badala ya uhaba.
👉🏽Upweke, kupata muda wa kukaa peke yako bila ya usumbufu wowote kunakupa nafasi ya kujitambua mwenyewe.
👉🏽Asili, kujumuika na asili kama kukaa au kutembea kwenye mazingira ya asili kunakupa utulivu mkubwa.
👉🏽Kusudi, kulijua na kuliishi kusudi la maisha yako kunakufanya uwe na msukumo mkubwa kiroho.
👉🏽Maana, kufanya kile chenye maana kwako na wengine kunakufanya usichoke kama unapofanya kisicho na maana.

Kazana kulisha roho yako kila siku kama unavyohangaika kulisha mwili wako, na nguvu utakayoipata itakuwezesha kufanya makubwa kwenye maisha yako.

Je umekuwa unalisha roho yako kila siku?
Kama hapana basi anza leo na utayaona manufaa yake.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu wanaofanya makosa kutokukamatwa, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/29/2099

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.