“The more a person expresses his love, the more people love him; and the more people love him, the easier it is for him to love others. In this way, love is eternal.” – Leo Tolstoy

Kadiri mtu anavyowapenda wengine, ndivyo wengine nao wanavyompenda zaidi.
Na kadiri watu wengi wanavyompenda mtu, ndivyo inavyokuwa rahisi kwake kuwapenda wengine.
Upendo ni mzunguko, upendo hauna ukomo.

Kama unaona watu hawakupendi, jiulize kwanza kama wewe unawapenda, kama unaonesha upendo kwao.
Upendo unaanza na wewe mwenyewe,
Kwa kuwapenda wengine kwanza,
Na kisha wao kukupenda.

Na wala usilazimishe upendo,
Wala usipende ili upendwe,
Wewe ufanye upendo kuwa msingi mkuu wa maisha yako,
Anza kwa kujipenda sana wewe mwenyewe,
Kisha wapende wote wanaokuzunguka,
Na pia penda kile unachofanya.

Upendo hauna gharama na wala hauchoshi, ila matunda yake ni yenye manufaa makubwa.
Upendo unakupa kujiamini, unakuweka huru kuyaishi maisha yako.

Kwa kuishi kwa upendo, utaweza kupunguza baadhi ya changamoto unazokutana nazo kwenye maisha yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kwa wengine ni mambo ya kawaida, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/02/2102

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.