“Nothing important comes into being overnight; even grapes and figs need time to ripen. If you say that you want a fig now, I will tell you to be patient. First, you must allow the tree to flower, then put forth fruit; then you have to wait until the fruit is ripe.” – Epictetus

Mafanikio ya haraka ni kitu ambacho hakijawahi kuwepo, hakipo na wala hakitakuja kuwepo.
Ni kitu kimekuwa kinatumika kuwahadaa na kuwatapeli wengine,
Kuibua hisia zilizo ndani yao ili wafanya maamuzi mabovu na yawanufaishe wengine.

Mambo mazuri yanahitaji muda, ndiyo maana unapaswa kuwa na utulivu na subira.
Huwezi kupanda mti leo halafu kesho utegemee kuvuna matunda.
Inahitaji muda kwa mti kukua, utoe maua kisha utoe matunda na yakomae kiasi cha kufaa kuliwa.

Bila kuwa na subira na uvumilivu, hutaweza kuyapata matunda hayo mazuri.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa mafanikio kwenye jambo lolote kwenye maisha yako, yanahitaji muda.

Muhimu ni kujua ni mafanikio gani unayotaka kufikia, kujua kazi unayopaswa kuiweka, kuweka kazi hiyo kila siku bila kuchoka, kisha kuwa na subira.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kauli ya kujijengea imani ya kupata unachotaka, isome hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/05/2105

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.