Watu wengi hufanya kilicho sahihi kwa sababu wana ajenda fulani, kuna kitu wanategemea kukipata kwa kufanya kilicho sahihi.
Hivyo wengi hufanya kilicho sahihi kama maigizo, haitoki kweli ndani yao, bali wanafanya kwa mategemeo fulani.
Lakini Mstoa Marcus Aurelius alituasa vyema, sababu pekee ya kufanya kilicho sahihi ni kwa kuwa ndiyo kitu sahihi kufanya.
Sijui umeelewa vizuri hapo rafiki yangu au unahitaji muda ili izame vyema, unafanya kilicho sahihi, siyo ili uonekane, au ulipwe kwa wema uliofanya, bali kwa sababu ndiyo kitu sahihi kufanya.
Mahali pengine Marcus alituonya kuhusu kusubiri shukrani pale tunapotenda kwa wengine. Alitueleza wazi kwamba faida ya kutenda wema tumeshaipata kwa kutenda wema huo, kusubiri shukrani ni kuharibu ole faida ambayo unakuwa umeshaipata.
Fanya kilicho sahihi kwa sababu ndiyo kitu sahihi kwako kufanya, huwezi kufanya mbadala na hicho sahihi. Fanya wema kwa sababu ndiyo namna sahihi kwako kuishi, huwezi kuishi kinyume na hivyo.
Kwa kifupi, kwa chochote unachofanya, kifanye kwa sababu ndiyo msingi wako wa maisha, na siyo kwa sababu unataka kuonekana au kuna kitu unategemea kupata kwa kufanya kitu hicho.
Kwa kuishi maisha yako hivi, utaondokana na msongo mwingi unaoletwa na mategemeo hewa ambayo wengi wamekuwa wanajijengea.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante hii ni makala moja nzuri sana kifalsafa kimaisha
Hii ni hata katika dini nyingi tulizo nazo licha ya wingi kwake lakini hatuoni watu wakizidi kuwa wema, wengi kuna ajenda wanayoifanya ili kupata kitu kupitia mgongo wa falsafa za dini.
Ukiishi kwa msingi wa kuwa ma wema kama ndiyo maisha na si kwa kutegemea kupata kitu fulani,hakuna wa kukuhubiria uwe mwema bali unasukumwa kufanya kwa kua ni muhimu kwako kufanya si kwa sababu ya…..
LikeLike
Hakika Hendry
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala nzuri za kistoa, hakika hakuna Sababu ya kusubili kulipwa kwa wema ambao umeutenda,siku moja tulikuwa kazini na kila siku asbh au jioni tunapewa maji sawa mawili mawili,mmoja akatoka kwenye gari anatamba amemuibia dereva maji yake,kilicho niuma ni mimi kujua kuwa huyu amemwibia wakati dereva analalamika aliemuibia maji yake,nilimuomba tumrudushie maji yake na ikawa hivyo.aAsante sana napenda haki na ukweli.
LikeLike
Asante Beatus kwa mfano huu mzuri unaoonesha nguvu ya hili.
LikeLike
“Nitafanya kwa sababu ni sahihi kwangu kufanya”
Shukrani sana kocha kwa makala nzuri.
LikeLike
Safi sana
LikeLike