“It’s not always that we need to do more but rather that we need to focus on less.” — Nathan W. Morris

Tunaishi kwenye zama ambazo kila mtu anasukumwa kufanya zaidi.
Lakini kadiri watu wanavyofanya mambo mengi zaidi, ndivyo wanavyochoka zaidi na kutokufanikiwa.

Kwa asili, matokeo makubwa hayatokani na kufanya vitu vingi zaidi, bali kufanya vitu vichache kwa ubora mkubwa.
Chukulia mwanga wa jua, ukitawanyika unatoa mwanga, lakini ukikusanywa pamoja unazalisha umeme (solar) au kuanzisha moto (kwa kutumia lensi)

Nguvu zinapotawanywa kwenye vitu vingi zinatoa matokeo hafifu,
Lakini zinapokusanywa kwenye vitu vichache zinazalisha matokeo makubwa mno.
Ni nguvu zile zile, kinachotofautiana ni namna zinavyotumika.

Asubuhi ya leo tafakari jinsi umekuwa unatawanya nguvu zako kwenye mambo mengi, kisha angalia matokeo gani umekuwa unapata.
Amua kuchagua mambo machache ambapo utakusanya nguvu zako ili uweze kupata matokeo makubwa zaidi.
Na kila unapotamani kufanya jambo jipya linalonyonya nguvu zako, kumbuka madhara ya kutawanya nguvu hizo.

Usihangaike na mengi, chagua machache muhimu na weka nguvu zako zote kwenye hayo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu njia ya uhakika ya kufika na kubaki kwenye utajiri, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/14/2145

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.