“Whosoever loves much performs much, and can accomplish much, and what is done in love is well done!” – Van Gogh

Yule mwenye upendo zaidi, anaweka juhudi zaidi na kuzalisha matokeo makubwa zaidi.
Kile kinachofanyika kwa upendo, kinafanyika kwa ubora wa hali ya juu.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, imani yetu kuu, kitu kinachotuleta pamoja ni UPENDO.
Hiyo ni kwa sababu UPENDO una nguvu ya kufanya mambo yasiyotegemewa.
Na UPENDO wetu umegawanyika kwenye maeneo matatu;
Eneo la kwanza ni upendo binafsi, kwa kujipenda sisi wenyewe, kujikubali na kujithamini. Tukijipenda tunakuwa bora zaidi.
Eneo la pili ni kuwapenda wale wanaotuzunguka, kwa kuwakubali walivyo na kushirikiana nao vyema. Kwa kuwapenda wengine, mahusiano yetu yote yanakuwa bora.
Eneo la tatu ni kupenda kile tunachofanya, kazi au biashara tunayofanya tunapaswa kuipenda sana, kwa kupenda tunachofanya, tunakifanya kwa ubora wa hali ya juu.

Kama hujipendi mwenyewe, huwapendi wanaokuzunguka na hupendi unachofanya, nafasi ya wewe kufanikiwa ni ndogo mno
Unaweza kubadili nafasi hiyo kwa kuanza na UPENDO.
Na Upendo hauhitaji kulazimisha, bali kujiachia na kujitoa kwa kile unachopata msukumo kutoka ndani yako, kuchagua kuyaishi maisha yako badala ya kuiga wengine na kujilinganisha nao.

Kila unapoamka jiambie NAJIPENDA, kila unapojikuta una wasiwasi au hofu jiambie NAJIPENDA.
Kila unapokutana na mtu yeyote, jiambie kimoyomoyo NAKUPENDA, hapa ni kwa wale ambao siyo wa karibu sana, labda wateja unaowahudumia au watu wengine unaokutana nao. Wale wa karibu waambie wazi mara nyingi uwezavyo, lakini kila wakati unapokutana na mtu mwingine kabla hamjafanya chochote, wewe jiambie NAKUPENDA na hilo litoke ndani yako kweli siyo kuigiza.
Kwa kila unachofanya, kabla hujaanza kukifanya jiambie NAPENDA kitu hiki. Iwe ni kazi au biashara, usianze kuifanya kabla hujajiambia unaipenda.
Fanya zoezi hili kila wakati na utaona mabadiliko makubwa yatakayotokea kwenye maisha yako, hutaamini kabisa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu unaweza kufanya kwa muda gani, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/15/2146

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.