“Words have more power than any one can guess; it is by words that the world’s great fight, now in these civilized times, is carried on.” – Mary Shelley

Maneno yana nguvu kubwa kuliko mtu yeyote anavyoweza kudhani.
Maneno yana nguvu ya kuumba chochote.
Maneno yameanzisha vita vilivyoua wengi, yamejenga uhasama mkubwa baina ya watu.

Lakini pia maneno yamejenga maelewano na utulivu mkubwa baina ya watu, yamewaponya watu na kuwapa furaha.

Unapaswa kutambua nguvu hii kubwa ya maneno kabla hujatumia neno lolote kwako binafsi na kwa wengine.
Tumia maneno ambayo ni chanya na yanayojenga.
Epuka maneno hasi na yanayobomoa.
Na tambua neno ukishalitoa, iwe ni kwa kuongea au kuandika, huwezi kulirudisha tena, huwezi kuzuia madhara yake.

Usitumie maneno hovyo, badala yake jua madhara ya kila neno kabla hujalitumia.
Tumia nguvu ya maneno kwa njia nzuri, kuboresha mawasiliano, kuimarisha mahusiano na kujihamaisha mwenyewe na wengine pia.

Tumia maneno chanya na yanayojenga matumaini kwako na kwa wengine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuchagua viwili kati ya rahisi, haraka na bora, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/18/2149

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.