“There is no deed in this life so impossible that you cannot do it. Your whole life should be lived as an heroic deed.” – Leo Tolstoy
Maisha siyo rahisi, kwa sababu huwa hayaendi kama tunavyopanga na kutaka.
Kila wakati unakutana na vikwazo na changamoto mbalimbali.
Ili uweze kufanikiwa, lazima uweze kuvuka vikwazo na kila aina ya changamoto unayokutana nayo.
Anza kwa kuamini kwamba hakuna lolote linaloweza kukushinda kwenye maisha yako.
Hata kama mambo ni magumu kiasi gani, unapojitoa kuyakabili, unayavuka na kuweza kusonga mbele.
Chagua kuishi maisha ya kishujaa, maisha yasiyoshindwa na chochote.
Unapoamua kile unachotaka, pambana mpaka ukipate.
Jiambie utapata kile unachotaka au utakufa ukiwa unapambana kukipata.
Ukijitoa kwa kiasi hicho, asili yenyewe itakuheshimu na kukupa kile unachotaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu nguvu unazozitawanya hivyo, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/19/2150
Rafiki yako anayekupenda sana.
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante sana kocha kwa tafakari hii, hakika kila hatua inayopigwa dhamila ya ndani au maandalizi yake inahitaji ushujaa.nipo tayari kuishi kishujaa ili kushinda vikwazo vitakavyojitokeza.
LikeLike
Hongera Beatus.
LikeLike