“The purpose of your life is not to do as the majority does, but to live according to the inner law which you understand in yourself Do not act against your conscience or against truth. Live like this, and you will fulfill the task of your life.” — Marcus Aurelius

Kusudi kuu la maisha yako siyo kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, bali kuishi kulingana na sheria ya ndani yako unayoielewa wewe mwenyewe.
Usiende kinyume na dhamiri yako au ukweli.
Kwa kuishi hivi utakamilisha kusudi la maisha yako na kuwa na maisha bora na yenye mafanikio.

Fanya kwa kuongozwa na vitu hivyo viwili; Dhamiri na Ukweli.
Dhamiri yako ndiyo inajua nini unataka na kipi muhimu kwako. Ukiiacha na kufuata wengine, unakuwa umejisaliti. Hivyo hata kama utapata wanachopata wengine, hutakifurahia, maana siyo dhamiri yako.

Ukweli ndiyo kitu muhimu, sahihi na kisicho adilika.
Mara nyingi kundi la wengi huwa halipendi ukweli, hasa unapokuwa mchungu, hivyo kwa kufuata kundi, unakuwa unapingana na ukweli.

Kila unalofanya jiulize je ni dhamiri yako? Inatoka kweli ndani yako au ni kwa sababu umeona wengine wanafanya?
Swali la kwanza likiwa ndiyo ni dhamiri yako, nenda kwenye swali la pili, je ni kweli?
Fanya kile tu kinachotokana na dhamiri yako na ambacho ni kweli, tofauti na hapo usifanye.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu msukumo wa ndani au wivu, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/22/2153

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.