“People who try to force circumstances become their slaves. Those who use them become their masters.” —The Talmud
“There is nothing in this world more tender and more pli able than water, yet hard and rigid things cannot resist it.” – Lao Tzu
Usilazimishe mambo yawe kama unavyotaka wewe,
Bali yatumie mambo jinsi yalivyo.
Unaweza kuwa na mipango mizuri sana.
Ukachukua kila hatua unayopaswa kuchukua.
Lakini matokeo unayopata yakawa siyo uliyotegemea.
Badala ya kutaka natokeo yawe kama unavyotaka, yatumie kwa namna sahihi.
Badala ya kuyakataa matokeo kwa kuwa siyo uliyotegemea, yakubali na uangalie jinsi ya kuyatumia vizuri.
Maji ni kitu chenye nguvu kubwa sana, lakini huwa hayalazimishi chochote.
Maji huwa yanakubaliana na kila hali, lakini katika kufanya hivyo yanakuwa na nguvu ya kubadili chochote.
Kuwa kama maji, kwa kuweza kuendana na kila hali na kuitumia kufanya makubwa zaidi.
Usipoteze muda na nguvu zako kutaka mambo yawe unavyotaka wewe,
Bali yakubali mambo jinsi yalivyo, kisha yatumie kufanya makubwa zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuanza na wewe, kisha soko, kisha biashara, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/29/2160
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.