“They who have decided to dedicate their lives to spiritual perfection will never be dissatisfied or unhappy, because, all that they want is in their power.” —Blaise Pascal
Kama unataka kuridhika na kuyafurahia maisha yako,
Basi jitoe kwa ajili ya ukuaji wa kiroho.
Unapojitoa kwa ajili ya ukuaji wa kiroho, unagundua kila unachohitaji tayari kipo ndani yako.
Huhitaji kutafuta chochote kutoka nje yako ndiyo ukamilike.
Hivyo ulivyo tayari umekamilika.
Jamii haipendi ujue hili, inajua ukijua umekamilika kwa jinsi ulivyo, haitaweza kukutumia na kukufanya mtumwa.
Hivyo imekuwa inakujaza ujinga,
Kwamba wewe siyo mkamilifu, kwamba chochote ulichonacho hakitoshi, kwamba ukipata kitu fulani ndiyo utakuwa na furaha.
Yote hayo ni uongo na njia ya kukufanya uendelee kuwa mtumwa kwa wengine.
Leo ni siku ya kujitangazia uhuru, siku ya kujua ulivyo umekamilika na kutumia kila kilicho ndanj yako kukua kiroho, kuwa huru na kuyafurahia maisha.
Hilo ndiyo jukumu kubwa na muhimu la maisha yako, ambalo linabeba majukumu mengine yote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kununua kabla hujauza, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/17/2178
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.