
Ni rahisi sana kuhamasika na kuamua kuchukua hatua kubwa mara moja.
Labda umesikia watu wenye mafanikio makubwa wanaamka mapema, saa tisa alfajiri na wewe ukaamua mara moja uanze kuamka saa tisa. Unaamka kwa siku chache lakini baadaye unashindwa.
Au unajifunza kuhusu umuhimu wa mazoezi, unahamasika na kuanza mazoezi, siku ya kwanza unakimbia km 5, siku inayofuata unajikuta una maumivu kila mahali kiasi kwamba huwezi kukimbia tena.
Ni vizuri kujifunza na kubadilika, lakini kuanza mabadiliko makubwa ambayo huwezi kuyamudu hakukusaidii.
Chochote unachopanga kufanya, hakikisha unaweza kumudu kukifanya kwa muda mrefu.
Hivyo kama ni kitu kipya kabisa anza kidogo kidogo na endelea kukua kadiri unakwenda.
Mafanikio siyo ushujaa wa siku moja, bali msimamo wa kufanya kitu kwa muda mrefu.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma