
Hadithi za utotoni zilikuwa zinamalizia na baada ya mateso wakaishi kwa raha mustarehe maisha yao yote. Hizo ni hadithi na siyo uhalisia.
Hakuna maisha ya raha muda wote, kila wakati kuna ugumu au changamoto unakabiliana nayo na ukivuka inakuja nyingine.
Furaha kwenye maisha ni kujua maana ya maisha yako, kujua kwa nini uteseke. Kutaka raha muda wote kumepelekea wengi kuharibu maisha yako, lakini kujua maana ya maisha, kumesaidia wengi kuyajenga.
Usihangaike na raha, hangaika na maana na raha zitakuja kwa wakati wake na kuondoka pia, ila kila unachokabiliana nacho, kitakuwa na maana na kitafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Furaha ni kama kipepeo, kadiri unavyoikimbilia ndivyo inavyokukimbia, lakini unapoyaishi maisha yako, inakuja kwako yenyewe.
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuingia na kukaa kwenye mstari wa mafanikio yako, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/17/2209
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma