
Watu wanaweza kufanya vitu ambavyo vinatushangaza, tukashindwa kuelewa kwa nini wamefanya hivyo. Ipo njia rahisi ya kuwaelewa watu kwa yale wanayofanya, ambayo ni kuangalia maslahi yao kwenye kile wanachofanya.
Kwa asili sisi binadamu ni wabinafsi, tunatanguliza maslahi yetu mbele kabla ya kingine chochote. Hivyo unapomuona mtu anafanya kitu, hata kama ni cha ajabu, jua kuna maslahi anayoyapata ndani yake.
Kwa kuyajua maslahi ya mtu, inakusaidia pia katika kuwashawishi au kuwabadili. Usiwashangae au kuwalaumu watu kwa wanayofanya kabla hujajua maslahi yao kwenye kufanya hivyo.
Ni vigumu sana mtu kufanya kitu kisichokuwa na maslahi kwake.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kinga ni bora kuliko tiba, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/02/2225
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma