
Mashine ya kwanza ya kushona nguo iliharibiwa vibaya na watu kwa sababu waliamini ni adui kwa ajira zao.
Tangu kuanza kwa ugunduzi wa mashine za kurahisisha kazi, watu wamekuwa wanazihofia na kuzipinga, kwa sababu ni adui anayechukua ajira nyingi.
Lakini kwa zama hizi hatuwezi tena vita hiyo, mashine zimeshakuwa sehemu ya maisha yetu. Na mashine za sasa ni janja, kwani zinaweza kuiga kila tunachofanya.
Kitu pekee ambacho haziwezi ni kuwa na utambuzi na ufahamu na kuwa na utu ndani yake. Vitu hivyo ndiyo vitaendelea kututofautisha binadamu na mashine.
Mashine zitaendelea kuwa hatari kwa wale wanaoishi kwa mazoea na kufuata mkumbo. Lakini kwa waliojitambua na kuishi maisha yao, mashine haziwezi kuwa hatari kwao, kwani zitakuwa zinawategemea ili ziwe na ufanisi.
Usikubali kuishi bila ya kujitambua, utakuwa mtumwa wa mashine na hata watu wengine.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kujua kila kitu, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/04/2227
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma