Chanzo cha wengi kuanguka na kukata tamaa ni kushikiza utu wao kwenye matokeo waliyopata au wanayotaka kuyapata.
Lakini matokeo huwa yako nje ya uwezo wa mtu kuyadhibiti na kuyaathiri. Hivyo mambo huwa hayaendi kama mtu anavyotegemea na hapo ndipo kuanguka na kukata tamaa kunapotokea.
Mahali sahihi pa kushikiza utu wako ni kwenye kusudi la maisha yako, kwenye hatua unazochukua na jinsi unavyoyaishi maisha yako. Kile unachofanya kipo ndani ya uwezo wako kuathiri na kudhibiti, unaweza kufanya vile unavyotaka.
Hivyo kwa kujiona kama mfanyaji, kwa kuishi vile ilivyo sahihi kwako, maisha yako yatakwenda vile unavyotaka. Lakini kwa kujipima kwa matokeo ambayo yako nje ya uwezo wako, utaishia kuanguka, maana hujui matokeo gani yatakuja.
Wajibu wako ni kufanya kile kilicho sahihi, matokeo yatakuja yenyewe kwa wakati wake. Iwe matokeo yatakuja au la, hilo halikuumizi, kwa sababu unachoangalia siyo matokeo, bali kile unachofanya.
Kile unachofanya kipo ndani ya uwezo wako, kudhibiti na kukifanya kwa usahihi. Matokeo unayoyataka yako nje ya uwezo wako, usiruhusu yakusumbue kwa namna yoyote ile.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante Sana kocha kwa makala.
LikeLike
Karibu.
LikeLike