
Unaweza kupata muda zaidi kwenye siku yako kama utaacha kuhangaika na yale yasiyo muhimu kwako.
Kuna mengi unajihangaisha nayo sasa ambayo hayana mchango wowote kwako, mfano kufuatilia maisha ya wengine.
Mstoa Marcus Aurelius amewahi kusema yule asiyehangaika na wengine wanafikiri, kusema au kufanya nini, ana muda mwingi wa kuhangaika na mambo yake.
Kama unalalamika huna muda, tambua kuna mahali unapoteza muda sasa, okoa muda huo na utaweza kuutumia kwa yale yaliyo muhimu kwako.
Ukurasa wa kusoma ni gharama ya utulivu wako wa akili, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/25/2248
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma