Watu wakitaka kuyavuruga maisha yako, wanaanza kwa kuvuruga akili yako.

Watu wakitaka kukuibia au kukutapeli, wanaanza kwa kuivuruga akili yako.

Na hata wale wanaotaka kukutumia kwa manufaa yao, wanahakikisha wamevuruga akili yako kwanza.

Akili yako ni rasilimali muhimu na yenye nguvu kubwa ndiyo maana ni kitu cha kwanza kushambuliwa.

Kila mtu anawinda umakini wako, kwani anajua akiwa nao, utakuwa tayari kufanya anachotaka.

Linda sana umakini wako na utulivu wa akili yako. Kuwa makini na usumbufu pamoja na mitego inayowekwa na wengine kuteka umakini na utulivu wako.

Fanya maamuzi yako muhimu ukiwa na utulivu mkubwa wa akili yako na maisha yako yatakuwa bora.

Ukurasa wa kusoma ni umuhimu wa kulinda juhudi unazoweka leo ili unufaike nazo baadaye, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/08/2259

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma