Mambo yanayokukabili sasa, yanakutosha kupambana nayo, ya nini ujiongezee mzigo kwa mambo ambayo bado hayajatokea?

Huwa tunapenda kuhofia mambo ambayo bado hayajatokea, lakini hofu hizo huwa hazisaidii chochote, zaidi ya kuwa kikwazo kwetu kukabiliana na yaliyo mbele yetu.

Yakabili yaliyo mbele yako sasa, peleka umakini wako wote hapo na yatakapokuja mengine, utayakabili kwa wakati yatakapokuja.

Usijisumbue na mambo ambayo bado hayajatokea.

Ukurasa wa kusoma ni umuhimu wa kupenda unachofanya, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/13/2265

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma