Kila unachosikia, kuona au kusoma, kuna ushawishi kinasababisha ndani yako. Hakuna kinachoingia kwenye akili yako bila kuacha madhara fulani.

Hivyo unapaswa kuwa makini sana na watu unaowasikiliza, unaowaangalia na unaowasoma. Wale wenye ushawishi usio mzuri kwako, kaa nao mbali sana.

Pia kuwa na msingi wako imara unaoufuata ambao mara zote unautumia katika kufanya maamuzi yako, hilo linazuia ushawishi wa wengine usikusukume kufanya maamuzi yasiyo sahihi kwako.

Ukurasa wa kusoma ni njia tatu za kuingiza kipato na tofauti zake; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/17/2299

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma