Huwa unaielewa asili na kwenda nayo kama inavyoenda. Hung’ang’ani kuilazimisha ibadilike na kwenda kama unavyotaka wewe.

Kama ulitaka sana jua liwake, lakini mvua ndiyo ikanyesha, huhangaiki kulazimisha jua liwake, bali unaenda na vile mvua inavyonyesha.

Lakini inapokuja kwa binadamu hufanyi hivyo, unataka wawe vile unavyotaka wewe, na kulazimisha kwa namna mbalimbali.

Kinachotokea ni hawawi unavyotaka, kitu kinachokukasirisha zaidi.

Hebu pata mfano unapita njiani na kukuta mtu ameshika jiwe na analia, unamuuliza kulikoni anakujibu ameliambia jiwe liwe mkate ili ale kwa sababu ana njaa, ila jiwe halijabadilika. Nadhani utamchukulia mtu huyo hayuko sawa kwenye akili.

Sasa usichojua hivyo ndivyo unavyokuwa pale unapotaka watu wengine wawe unavyotaka wewe.

Ukurasa wa kusoma ni jumbe zinazokinzana; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/20/2302

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma