
“Mostly it is loss which teaches us about the worth of things.” – Arthur Schopenhauer
Kwenye maisha ya kawaida huwa tunathamini zaidi vitu ambavyo kuna hatari ya kuvipoteza. Mfano ukiambiwa ofa ya kitu inaisha, unakithamini zaidi na kuhakikisha unakipata.
Lakini inapokuja kwenye maisha yako mwenyewe, mbona hutumii hilo? Mbona upoteze muda kwa mambo yasiyo na tija wakati unajua muda huo hutaupata tena kwenye maisha yako?
Kithamini kila kinachopotea na kukitumia kwa manufaa, ukianza na maisha yako mwenyewe.
#MementoMori #ThaminiKinachopotea #KochaMakirita