Maisha ni kama ligi ya mpira, timu inayochukua kombe siyo inayoshinda michezo yake yote, bali inayoshinda michezo iliyo mingi, tena ile ya muhimu.

Kwa kujua hilo, ili timu ishinde inapaswa kujipanga na kujua michezo ipi lazima ishinde na ipi hata ikishindwa siyo mbaya, hilo linasaidia timu ipangilie rasilimali zake vizuri.

Kwenye maisha yako hupaswi kupambana na kila kitu ili kukishinda, bali unapaswa kupambana na yale muhimu zaidi.

Yasiyo muhimu yaache, hata yakikushinda siyo tatizo, lengo lako siyo kushinda kila pambano, bali kupata ushindi mkuu.

Na huo utaupata kwa kupangilia vizuri rasilimali zako za mapambano, kuchagua kushindwa baadhi ya mapambano ili ushinde mengine muhimu zaidi.

Ukurasa wa kusoma ni ushujaa siyo kupambana pekee; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/22/2334

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma