
Hebu fikiria umekaa mwezi mzima bila kula chakula kabisa, mwili wako utakuwa katika hali gani? Vipi ukikaa mwezi mzima bila kuoga kabisa?
Hutafikisha hata mwezi, mwili utakuwa umeharibika kabisa. Sasa pata picha ni kwa kiasi gani unaharibu akili yako kwa kutokuilisha chakula sahihi.
Matokeo ya mwili yanaonekana haraka kwa sababu unaona mwili kwa nje, matokeo ya akili hayaonekani haraka kwa sababu huioni akili. Lakini matokeo yako wazi, maisha uliyonayo sasa ni matokeo ya kile ulicholisha akili yako.
Kama unataka maisha ya tofauti, lazima ulishe akili yako maarifa ya tofauti. Usikubali kupata muda wa kufanya kila kitu halafu ukose muda wa kusoma vitabu, unakuwa umechagua kuwa na mtindio wa ubongo.
Ukurasa wa kusoma ni maisha kama kombolela; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/26/2338
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Asante Sana kocha kwa tafakari hii, nakumbuka mara ya kwanza najiunga kcm nilisema sina muda wa kusonga vitabu, uliniomba nikupe ratiba yangu ya siku,kwa sasa nasoma vitabu vzr, hakika wewe ni mwalimu,kocha wa mfano, nitaendelea kupambana kwa jasho na damu ili kweli lengo la kisima cha Maarifa lifanikiwe kupitia mimi.
LikeLike
Asante na karibu sana Beatus.
LikeLike