Hebu fikiria umekaa mwezi mzima bila kula chakula kabisa, mwili wako utakuwa katika hali gani? Vipi ukikaa mwezi mzima bila kuoga kabisa?

Hutafikisha hata mwezi, mwili utakuwa umeharibika kabisa. Sasa pata picha ni kwa kiasi gani unaharibu akili yako kwa kutokuilisha chakula sahihi.

Matokeo ya mwili yanaonekana haraka kwa sababu unaona mwili kwa nje, matokeo ya akili hayaonekani haraka kwa sababu huioni akili. Lakini matokeo yako wazi, maisha uliyonayo sasa ni matokeo ya kile ulicholisha akili yako.

Kama unataka maisha ya tofauti, lazima ulishe akili yako maarifa ya tofauti. Usikubali kupata muda wa kufanya kila kitu halafu ukose muda wa kusoma vitabu, unakuwa umechagua kuwa na mtindio wa ubongo.

Ukurasa wa kusoma ni maisha kama kombolela; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/26/2338

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma