Ukitaka kujisikia vizuri, sikiliza uongo, maana huo unakubembeleza na haukuumizi.

Ukitaka kuwa bora sikiliza ukweli, huo hakubembelezi na unakuumiza.

Walio wengi wanapenda kubembelezwa na kutokuumizwa, ndiyo maana hawapigi hatua kwenye maisha yao.

Ni wachache sana walio tayari kuukabili ukweli unaowaumiza na usiowabembeleza, lakini unawafanya kuwa bora zaidi.

Kama unataka kufanikiwa, kuwa tayari kuukabili ukweli unaouma.

Ukurasa wa kusoma ni mrejesho ni zawadi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/01/2374

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma