
Jamii imekutengenezs kuhofia mambo yasiyo na tija yoyote kwako. Mfano kuhofia wengine wanakuchukukiaje, kuhofia kukosolewa na hata kuhofia kupitwa na yanayoendelea kwenye mitandao.
Hofu zote hizo hazina manufaa yoyote kwako. Ili kuziondoa zisiwe kikwazo, zigeuze kuwa furaha. Furahia pale wengine wanapokupinga au kukukosoa na kama ni watu sahihi jifunze kwao, kama siyo watu sahihi wapuuze.
Furahia kupitwa na yanayoendelea mitandaoni, ukijua unakazana na yake muhimu zaidi kwako, ambayo huwezi kuyapata mtandaoni.
Unapoacha kusumbuliwa na hofu hizo ndogo ndogo, unatengeneza uwanja mpana wa wewe kuchukua hatua sahihi ili uweze kufanikiwa.
Ni hofu gani zimekuwa zinakukwamisha sana? Zijue na uzigeuze sasa kuwa furaha kwako na usonge mbele badala ya kukwama.
Ukurasa wa kusoma ni furahia kupitwa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/10/2383
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma