
Watu wengi hawanufaiki na yale wanayosoma, kwa sababu shule zimewaharibu.
Shuleni mtu alisoma ili kufaulu mtihani, mtihani ukishapita basi hajali tena yale aliyosoma.
Kwenye maisha husomi ili kujibu mtihani, bali unasoma ili kuyafanya maisha yako kuwa bora.
Hivyo kwa kila unachojifunza, unapaswa kukitafakari ba kuona jinsi ya kukitumia kwenye maisha yako ili yawe bora zaidi.
Usifurahie tu kusoma, bali chukua hatua kupitia yale unayojifunza.
Ukurasa wa kusoma ni kula na Kumeng’enya; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/12/2385
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
kweli kocha,wengi wangejua hili wala wasingebeza kukuona na kitabu.Wengi wakikuona unasoma kitabu cha siri za mafanikio wataponda we kwamba hayo mavitabu yanawapoteza lakini ukimuangalia anepondea hivyo kwamba havimsaidii kitu utakuta ana matatizo kibao.
Tusome vitabu vinavyoweza kutatua changamoto tunazopitia kwa kuyatekeleza uliyojifunza badala kufurahia kumaliza kusoma
LikeLike
Kweli kabisa Hendry
LikeLike
Kwwli kocha ninapaswa kusoma ili kuyafanya maisha yangu kuwa Bora NA sio kujibu mtihani natahakikisha niliyojifunza na kila nitakachojifunza nitajiuliza kuwa nawezaje kukitumia kwenye maisha yangu yaweze kuwa Bora.
LikeLike
Vizuri James.
LikeLike