Watu wengi hawanufaiki na yale wanayosoma, kwa sababu shule zimewaharibu.

Shuleni mtu alisoma ili kufaulu mtihani, mtihani ukishapita basi hajali tena yale aliyosoma.

Kwenye maisha husomi ili kujibu mtihani, bali unasoma ili kuyafanya maisha yako kuwa bora.

Hivyo kwa kila unachojifunza, unapaswa kukitafakari ba kuona jinsi ya kukitumia kwenye maisha yako ili yawe bora zaidi.

Usifurahie tu kusoma, bali chukua hatua kupitia yale unayojifunza.

Ukurasa wa kusoma ni kula na Kumeng’enya; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/12/2385

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma