Muda na nguvu zako ni rasilimali muhimu sana kwako. Namna unavyochagua kutumia rasilimali hizo ni juu yako mwenyewe.

Wapo wanaozitumia hovyo na kuzipoteza na wapo wanaozitumia vizuri na kunufaika.

Wewe chagua kutumia rasilimali hizo vizuri, kwa kuhakikisha unaziwekeza kwenye kufanya mambo yenye tija kwako na kwa wengine pia.

Iwe utachagua kufanya mazuri au mabaya, muda na nguvu utakazotumia ni zile zile.

Hivyo ni vyema uchague kutumia kwenye mazuri, ili upate manufaa.

Ukurasa wa kusoma ni juhudi ni zile zile; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/14/2387

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma