Kwa chochote unachotaka kufanya, huhitaji taarifa zaidi ndiyo uanze. Tayari unazo taarifa za kukutosha kuanza kufanya.

Ukijiambia unasubiri mpaka upate taarifa za kutosha, utakuwa unajidanganya.

Unachopaswa ni kuanza kwa taarifa ambazo tayari unazo, na kisha kuendelea kujifunza kadiri unavyokwenda.

Tunaishi kwenye zama za mafuriko ya taarifa, ni rahisi sana kuzama kwenye taarifa mpaka kupoteza mwelekeo.

Lakini ukiwa umeshaanza kufanya, utajua ni taarifa zipi utafute. Kwa vyovyote vile, anza kufanya, usizuiwe na kukosa taarifa.

Ukurasa wa kusoma ni tayari una taarifa za kutosha; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/22/2395

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma