Kama unataka kubadili matunda ambayo mtu unazalisha, kukata matawi hakutasaidia. Unapaswa kung’oa kabisa shina la mtu huo na kupanda mti mwingine.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mabadiliko ya maisha yetu. Hutaweza kuyabadili maisha kwa kuhangaika na tabia pekee, bali anza kwa kubadili imani ya ndani yako.

Tabia ulizonazo ni matokeo ya imani hiyo, na tabia ndiyo zinajenga maisha yako. Ukibadili imani ya ndani, tabia zinabadilika na maisha yanabadilika pia.

Ukibadili tabia bila kugusa imani, mabadiliko yanakuwa ya muda mfupi ila baadaye unarudi kwenye tabia zile zile, maana imani ina nguvu kubwa.

Anza na imani, hicho ndiyo kiini cha mabadiliko.

Ukurasa wa kusoma ni kwa nini mabadiliko yanakuwa magumu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/27/2400

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma