Hisia zako ndizo zinahusika kwenye maamuzi yote unayofanya.

Unaweza kujiambia umetumia fikra, lakini ulichofanya kwenye fikra ni kuzihalalisha hisia zako.

Bila hisia ni vigumu sana kufikia maamuzi yoyote yale, maana utatumia muda mwingi kuchambua kila chaguo kililopo.

Lakini kwa hisia utachagua kile unachopenda kisha kuhalalisha kwa fikra kwamba ndiyo maamuzi sahihi kwako.

Kwa kuwa huwezi kubadili hili, unachopaswa kufanya ni kudhibiti hisia zako, ili ziweze kufanya maamuzi bora.

Ukurasa wa kusoma ni hisia, hadithi na mantiki; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/28/2401

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma