
Majaribu huwa yanapima msimamo ambao mtu anao kwenye jambo lolote lile.
Ambao hawajawahi kupitia majaribu makubwa kwenye kitu, wanaweza kudhani wana msimamo, kumbe siyo.
Huwa tunawashangaa watu kwamba wamebadili msimamo wao, kwamba awali walikuwa na msimamo fulani, ila baada ya kupata fursa fulani wakabadilika.
Hao hawakuwa na msimamo, ila tu walikuwa hawajakutana na fursa za kupima kile walichodai ni msimamo kwao.
Ni sawa na mtu asiye na uwezo wa kununua gari anaposema gari siyo muhimu, ila akiwa na uwezo analinunua. Siyo msimamo, ni kukosa fursa.
Tambua watu na hata wewe mwenyewe unaposimama, ni kwenye msimamo au kukosa fursa?
Ukurasa wa leo ni msimamo na fursa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/03/2407
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma