Kutumia hovyo rasilimali ambazo zina uhaba mkubwa ni kikwazo kwako kuweza kupiga hatua na kufanikiwa.

Kwa rasilimali hizo muhimu, unahitaji ubahili na ufanisi. Ubahili katika kutumia ili zitoshe na ufanisi katika kutumia ili zilete matokeo makubwa.

Rasilimali ulizonazo tayari zinakutosha kupiga hatua kubwa, kama unaona hazitoshi ni kwa sababu huna ubahili na ufanisi.

Anza na hayo mawili na utaona jinsi rasilimali ulizonazo zinavyotosha kufanya makubwa.

Ukurasa wa kusoma ni ubahili na ufanisi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/08/2412

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma