2414; Ukishindwa, usiwajibie wengine…
Nimekuwa nasema kama kuna kitu unatumia kama sababu ya kushindwa kupata unachotaka, lakini kuna mwingine ameweza kupata licha ya kuwa na hiyo wewe unaita sababu basi siyo sababu kweli, ni kisingizio tu.
Moja ya dalili za kushindwa bila kukubali ni kuwa tayari kuwajibia wale walioweza, kwa kuonyesha kwa nini wao wameweza ila wewe umeshindwa.
Mfano ni pale unasema umeshindwa kuanza biashara kwa sababu huna mtaji, ila wengine walioweza kuanza unawajibia kwamba walisaidiwa, au wanatoka familia nzuri, na mengine mengi.
Ukweli ni kwamba majibu yoyote unayojaribu kuwajibia wengine, ili kuhalalisha kushindwa kwako kwa yale ambayo wao wameshinda, ni kujidanganya tu.
Kama umeshindwa, kushinda kwa wengine hakuna uhusiano na kushindwa kwako.
Ukiacha kujipa majibu na ukajifunza kwa hao wengine utaweza kupiga hatua kubwa.
Ukishindwa, usiwajibie wale walioshinda, bali jifunze kutoka kwao.
Kushindwa ni kushindwa, usijaribu kuficha kushindwa kwako nyuma ya mgongo wa wengine.
Kushindwa siyo kubaya kama unajifunza na kuchukua hatua. Lakini kama unakimbilia kutafuta visingizio, kushindwa kunakuwa mzigo mkubwa kwako.
Kocha.