Rafiki yangu mpendwa,
Sasa hivi haihitajiki tena nguvu kubwa kukushawishi kwamba njia ya uhakika ya kuingiza kipato ni kupitia biashara.

Kwa miaka ya nyuma ajira ndiyo zilikuwa njia ya uhakika na watu walishawishiwa kusoma ili kuzipata.

Lakini pamoja na wengi kusoma, nafasi za ajira zimekuwa finyu na wengi hawazipati.

Na hata kwa wachache wanaozipata, hawazifurahii wala kunufaika nazo, hasa kifedha.

Hivyo iwe una ajira au huna, unapaswa kuwa na biashara.
Nimekuwa nasisitiza sana hili, kwa zama tunazoishi sasa, usikae huna kitu unachoweza kuwauzia wengine ambacho hakuna anayekupangia jinsi ya kukifanya.

Naamini sana kwenye biashara na ujasiriamali na najua ndani yetu kila mmoja ni mjasiriamali.
Na ndiyo maana nimekuwa naweka juhudi kubwa kwenye kukuandalia maarifa ya kukusaidia kwenye hilo.

Mfano kwenye kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, nimekuonyesha jinsi ambavyo kila mtu anaweza kuanzisha na kukuza biashara yake huku akia ameajiriwa.

Ni kitu ambacho wengi wamekuwa wanaona hakiwezekani na kutumia visingizio vingi, lakini kitabu kimejibu yote hayo.
Kama bado hujakisoma, kipate leo kwa kuwasiliana na 0752 977 170.

Kitu kikubwa ninachoshukuru ni kwamba watu wamekuwa wanapata maarifa ninayoshirikisha na wanachukua hatua.

Lakini mambo huwa hayawi rahisi, kwani kila hatua mpya ambayo mtu anachukua, inatengeneza changamoto mpya ambazo hazikuwepo hapo awali.

Changamoto hizo zimekuwa zinawakuta watu wakiwa hawajajiandaa na hivyo kupelekea wengi kutaka kukata tamaa.

Lakini mimi nipo na wewe, nikihakikisha kila unachokianza kinafanikiwa kabia na ninazo huduma mbalimbali za kukusaidia kwenye hilo.

Moja ya maeneo ambayo watu wanatengeneza changamoto mpya ni kwenye biashara.

Baada ya mtu kuhamasika na kuchukua hatua ya kuanza biashara, ndiyo anazifungua changamoto mpya ambazo hajawahi kukutana nazo kwenye maisha yake.

Na changamoto moja kubwa ambayo wengi hukutana nayo ni masoko.
Kuanza biashara ni rahisi, hasa kwa zama hizi ambapo mtandao wa intaneti umerahisisha mengi.

Lakini kuwashawishi watu wanunue, wakupe fedha zao ambazo wamezitafuta kwa jasho siyo rahisi.
Lakini pia urahisi wa kuingia kwenye biashara umetengeneza ushindani mkali sana.
Hivyo wafanyabiashara wengi mnakuwa mnagombania wateja wale wale.

Kwa sababu hizo basi, nimekuwa nawashauri wote walio kwenye biashara au wanaopanga kuingia kwenye biashara kuweka nguvu zao kubwa kwenye masoko.

Masoko ndiyo eneo linaloweza kujenga au kuvunja biashara yako.
Bila masoko hakuna wateja na bila wateja hakuna biashara.
Hivyo tunaweza kusema masoko ndiyo biashara yenyewe.

Hata kama una bidhaa au huduma nzuri kiasi gani, kama watu hawajui uwepo wako na jinsi gani wananufaika, hawatakuja kununua na biashara haitakupa manufaa.

Kuna mambo makubwa mawili ya kufanya kwenye masoko ili biashara yako iweze kukua.

Jambo la kwanza ni kutoa thamani kubwa sana ambayo mteja hawezi kuipata mahali pengine popote.

Fedha ni rasilimali yenye uhaba na hivyo kila mtu anapima kabla hajatumia fedha yake.
Mtu akishatumia fedha kwenye kitu kimoja, hawezi tena kuitumia kwenye kitu kingine.

Hivyo watu huwa hawatumii fedha zao mpaka wahakikishe ndiyo matumizi bora kabisa wanayoweza kufanya kwa fedha zao.
Na hapo ndipo penye fursa ya kuwapata wateja na kuwashawishi kununua.
Toa thamani kubwa mno, thamani ambayo mteja hawezi kuipata kokote, thamani ambayo mteja anaona kama amekuibia.

Yaani mfanye mteja aone hapotezi fedha yake, bali anaitumia kwa namna sahihi kabisa kwake.

Unaijua biashara yako vizuri, angalia ni kwa namna gani unaweza kumpa mteja wako thamani kubwa na akawa tayari kununua.

Kama huoni hilo kwenye biashara yako, tuwasiliane kwa wasap 0717 396 253 na tutajadiliana kwa ufupi uweze kujua thamani kubwa unayoweza kuwapa wateja wako.

Jambo la pili ni kukamata hisia za wateja wako.
Sisi binadamu ni viumbe wa hisia, huwa tunafanya maamuzi yetu kwa kusukumwa na hisia na baadaye kuyahalalisha kwa fikra na mantiki.

Kama unataka watu wanunue unachouza, acha kuhangaika na mantiki, wewe hangaika na kugusa hisia zao.

Kuna hisia kuu mbili za kugusa kwa wateja wako; maumivu na tamaa.

Maumivu ni hisia yenye nguvu, mwonyeshe mteja ni nini anachokosa sasa au atakachokosa kwa kutokununua kile unachouza.
Ukiweza kugusa maumivu sahihi, wateja watakukimbilia kukupa fedha zao.

Tamaa ni hisia nyingine unayoweza kuigusa na ikawasukuma wateja kununua. Kwenye tamaa unawaonyesha wateja mazuri ambayo watayapata na yatakavyonufaisha maisha yao.

Kwa sababu watu wanapenda vitu vizuri, watakuwa tayari kununua.

Ukitumia hisia hizo mbili kwa pamoja, yaani maumivu na tamaa, ushawishi unakuwa mkubwa kuliko ulitumia moja.

Kitu kimoja ninachoweza kukuambia ni hiki, kila biashara ina namna ya kutumia hisia na maumivu kuwashawishi wateja wake kununua.
Je huoni namna gani biashara yako inaweza kufanya hivyo? Tuwasiliane kwa wasap 0717 396 253 na nitakuonyesha.

Rafiki, usikubali kuendelea tena kuteseka na biashara kwa kutokupata wateja wa kutosha, weka nguvu zako kwenye masoko na utavuna matokeo mazuri.

Na kama unahitaji njia za uhakika za kujenga mfumo wa masoko kwenye biashara yako, tuwasiliane kwa wasap 0717 396 253 na tutalifanyia kazi hilo kwa pamoja.

Usikose kusoma kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA ambacho kitakupa mwongozo zaidi kwenye eneo la masoko. Wasiliana na 0752 977 170 kupata nakala yako ya kitabu.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz