
Maisha huwa hayasimami, mara zote yanaenda mbele. Na wewe pia hupaswi kusimama, mara zote nenda mbele.
Iwe utaruka, kukimbia, kutembea au kutambaa, wewe songa mbele. Hiyo ndiyo njia pekee ya kujisogeza karibu na kile unachotaka.
Pambana usonge mbele, kila siku jifunze na fanya kitu kipya ambacho hujawahi kufanya huko nyuma.
Usikubali siku zako mbili zifanane, usikubali kuendesha maisha yako kwa mazoea. Kila unachofanya kila siku, kinayaathiri maisha yako.
Fanya kile ambacho kina manufaa ya kweli na kukufikisha kwenye mafanikio unayoyataka.
Ukurasa wa kusoma leo ni ubaya ni kusimama; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/09/2413
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma