Unaweza kutoa motisha kwa nia njema kabisa, ili kuwasukuma watu wafanye kile unachotaka wafanye.

Maana binadamu kwa asili ni wavivu na wazembe, bila motosha ni vigumu sana kufanya kitu.

Lakini pia binadamu ni wajanja, wanaweza kuuchezea mfumo wowote ule ili waweze kujinufaisha zaidi. Hivyo kama unatoa zawadi, wanatafuta njia ya kuipata hata kama hawakidhi vigezo.

Na kama unatoa adhabu wanatafuta njia ya kuikwepa adhabu hiyo hata kama wamefanya makosa yanayostahili adhabu.

Kabla hujatumia motisha, jua mianya yote inayoweza kutumiwa na watu kujinufaisha zaidi na uizibe. Lengo ni motisha uweze kuleta matokeo mazuri unayotaka.

Ukurasa wa kusoma ni adhabu na zawadi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/11/2415

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma