Rafiki yangu mpendwa,
Tunaishi kwenye zama za taarifa.
Zama ambazo wale wenye maarifa na taarifa sahihi ndiyo wanaoweza kufanya maamuzi sahihi na kunufaika.

Uzuri wa zama hizi ni kwamba taarifa na maarifa ni mengi mno na yanapatikana bure kabisa kupitia mtandao wa intaneti.
Chochote kile unachotaka kujua, basi tayari kipo kwenye mtandao wa intaneti.

Hakuna kitu chochote kile ambacho huwezi kukipata kwa kutafuta kwenye google. Na hiyo google ni bure kabisa kutumia.

Lakini kuna tatizo moja kubwa, maarifa yaliyo kwenye google ni mengi kiasi kwamba yanakuchanganya kuliko kukusaidia.

Chochote utakachotafuta kwenye google, utetewa mamilioni ya majibu ambayo huwezi kuyapitia yote na hata utakayoweza kupitia yanaweza kuwa yanakinzana.

Hilo limekuwa linawapotezea watu wengi muda kwa kuhangaika na taarifa nyingi ambazo hazina manufaa kwao.
Huwa naita ni kuzama kwenye mafuriko ya taarifa, au kufa kwa kiu ukiwa kwenye kisima cha maji.

Kutokana na changamoto hii ya watu kukosa maarifa na taarifa sahihi kwao kutoka kwenye mtandao wetu pendwa wa kutafuta chochote ambao ni google, nimeona kuna fursa ya kutengeneza google maalumu ya mafanikio.

Google ya mafanikio ni mfumo wa kushirikishana uzoefu halisi kitu ambacho kina manufaa kuliko mafuriko ya taarifa mtandaoni.

Kwa kujifunza kutoka kwa mtu ambaye amekifanya kitu, unaondoka na taarifa na maarifa ambayo unaweza kuyafanyia kazi mara moja na siyo kuendelea kusubiri kwa sababu unaona bado hujajua.

Wakati napata wazo hili niliangalia na kuona tayari tunao watu wenye uzoefu mkubwa kwenye eneo la mafanikio kupitia KISIMA CHA MAARIFA.
Tayari tunao uzoefu mwingi wa mengi ambayo watu wamekuwa wakijaribu na kujifunza mengi.

Kinachohitajika ni kuyakusanya vizuri maarifa na taarifa hizo kwa namna ambayo kila mtu anaweza kuzitumia kwa manufaa zaidi.

Kupitia huduma hii ya KISIMA CHA MAARIFA ninayotoa, nimebahatika kujua mengi ambayo watu wanafanyia kazi, yale waliyoshindwa na yale waliyofanikiwa.

Kama changamoto yako ni kushindwa kuanza biashara ukiwa kwenye ajira, wapo wengi ambao wameweza kufanya hivyo, wakakuza biashara zao na kuweza kuondoka kwenye ajira.

Kama changamoto yako ni kukosa mtaji wa kuanza biashara, ipo mifano ya walioweza kuanza biashara bila ya mtandao na walioweza kukusanya mtaji na kuanza biashara.

Kama changamoto yako ni kipato kutokutosheleza, kuwa na madeni na kukosa akiba na uwekezaji, wapo waliokuwa hapo ulipo sasa na wakaweza kutoka.

Kama changamoto yako ni kustaafu huku ukiwa hujui utafanya nini na maisha yako, wapo ambao wamepita njia hiyo na mambo yao kwenda vizuri.

Kikubwa ambacho nimejifunza kupitia wale ninaofanya nao kazi kwa karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni changamoto za safari ya mafanikio ni zile zile.
Hakuna ambazo ni mpya, hivyo mtu akipata nafasi ya kujifunza kupitia uzoefu wa wengine, inakuwa na manufaa kwake kuliko kuhangaika na mafuriko ya taarifa mtandaoni.

Na hapo ndipo ninaokualika tufanye kazi pamoja ya kuijenga ‘GOOGLE YA MAFANIKIO’ ambao ni mtandao wa kushirikishana uzoefu ambao kila mtu anao kwenye eneo la mafanikio.

Uzoefu haimaanishi tu kupata matokeo mazuri, bali pia kupata matokeo mabaya ni uzoefu. Unapojifunza kwa waliokosea, unaepuka kurudia makosa yao na hivyo kuokoa muda wako zaidi.

Kwa muda nimekuwa nakusanya uzoefu huo kwa kutoa kwa mtu mmoja na kupeleka kwa mtu mwingine.
Lakini sasa nakwenda kuliweka hili wazo, ili kila mmoja aweze kupata maarifa, taarifa na uzoefu wowote anaotaka kutoka kwa wengine.

Kwa mfano kwenye kipindi cha live cha ONGEA NA KOCHA ambacho naendesha kwenye KISIMA CHA MAARIFA, baada ya kuongea na baadhi ya wanamafanikio walioshirikisha safari zao za kibiashara, nimeona mwamko mkubwa mno kwa wengine kutaka kukuza biashara zao.

Hata ambao walikuwa wanatoa visingizio mbalimbali kwa nini hawawezi kuanza biashara, sasa wanaona wazi kwamba walikuwa wanajizuia wao wenyewe.

Hili limenifanya nione kuna thamani kubwa kwenye uzoefu mkubwa wa wengine ambao tayari upo.
Kinachohitajika ni kuukusanya vizuri ili kila anayehitaji aweze kupata na kutumia.

Vitu viwili unavyohitaji ili kuwa sehemu ya ‘Google ya mafanikio’ ni;
1. Kuwa mwanachama hai wa KISIMA CHA MAARIFA na unayeshiriki kwenye huduma mbalimbali zilizopo kwenye KISIMA.
2. Kushiriki semina ya kukutana ana kwa ana kila mwaka, ambapo kunakuwa na mwongozo wa kufanyia kazi kwa mwaka mzima ili kuendelea kujenga na kushirikishana uzoefu ambao tunaendelea kuukusanya.

Kwa mfano semina ya mwaka huu 2021 itafanyika Oktoba 16 na 17 jijini Dodoma na katika semina hii ndiyo tutazindua rasmi ‘GOOGLE YA MAFANIKIO’.
Tutakuwa na mwongozo maalumu wa kufanyia kazi mwaka mzima ili kuweza kushirikiana kwa karibu na kupiga hatua kubwa kimafanikio.

Kama bado hujathibitisha kushiriki semina hii, fanya hivyo leo hii kwa kutuma ujumbe kwenda namba 0717 396 253.
Kuna maandalizi muhimu nahitaji kufanya kwa ajili ya wale tu watakaoshiriki, hivyo thibitisha mapema leo ili uwe sehemu ya maandalizi hayo.

Kama ilivyo kauli maarufu, wapumbavu huwa hawajifunzi kabisa, wajinga hujifunza kwa uzoefu wao wenyewe na werevu hujifunza kwa uzoefu wa wengine.
Karibu kwenye GOOGLE YA MAFANIKIO ili uweze kujifunza kutoka kwenye uzoefu wa wengine, uokoe muda na nguvu ambazo ungepoteza kwa kujifunza kwa uzoefu wako au kukusanya taarifa mitandaoni.

Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA wasiliana na mimi kwa namba 0717 396 253 na nitakupa maelekezo ya kujiunga.
Kama umeshakuwa mwanachama waalike watu wako wa karibu ili nao wajiunge na kunufaika na haya.

Kwa pamoja tunakwenda kutengeneza mfumo mzuri wa kushirikishana uzoefu ili kuweza kupiga hatua zaidi.
Karibu uwe sehemu ya zoezi hili kubwa na lenye manufaa kwa kila mmoja wetu.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz