2423; Hakuna mawazo yako peke yako…
Umewahi kupata wazo la kitu fulani, labda ni fursa nzuri umeiona na kujiambia utafanyia kazi baadaye.
Halafu siku si nyingi unakuta watu wengine wameshafanyia kazi wazo hilo hilo?
Hilo hutokea kila mara.
Wakati mwingine unamwambia mtu kitu anakuambia alikuwa anafikiria hivyo hivyo.
Mawazo tunayoyapata yanatokana na mawimbi yanayouzunguka ulimwengu.
Ni kama yalivyo mawili ya redio, ukiweka namba fulani redio inanasa mawimbi na kusikia sauti.
Hivyo ukiwa kwenye hali fulani, unanasa mawimbi ya mawazo unayokuwa nayo.
Haimaanishi ni wewe peke yako umenasa mawimbi hayo, wapo wengine pia ambao wameyanasa.
Hivyo unapopata mawazo mazuri, jua kabisa siyo wewe peke yako umeyapata, wapo wengine wengi walioyapata.
Njia pekee ya kunufaika na mawazo mazuri unayoyapata, ni kuyafanyia kazi. Unaposubiri, unawapa wengine nafasi ya kuwahi kuyafanyia kazi.
Kocha.
Kweli kabisa kocha.
LikeLike